|
Kwa kuwa tumezaliwa binadamu ni wajibu wetu sisi sote kutafakari kwa njia iliyo sahihi na kuamua njia ya kwenda. Tumo humu Duniani kwa majaribio ili kwamba wake watakaoshinda mtihani huu vizuri zaidi wazawadiwe za kushangaza kutoka kwa Muumba na mstawishaji wetu katika siku ya hukumu. Na ni dhahiri kuwa ni wale tu wenye akili ndio watakaoshinda mtihani huu. Hivyo basi ni muhimu kutumia zawadi ya Mwenyezi Mungu ya akili kwa makini sana majaaliwa haya kutoka kwa Mwenyezi Mungu (S.W.T) mwenye bahati ni yule anaeiendeleza na mkosefu ni yule ambae hatambui thamani yake
|